Serikali na Wabunge walio mstari wa mbele kwenye kutoa msukumo juu ya uimarishwaji wa afua za kutokomeza Usugu wa Dawa (AMR) wamekubaliana kuanzisha mfumo endelevu wa kufadhili afua za kukabili usugu wa vimelea dhidi ya dawa.
Kikao hicho muhimu kimefanyika Desemba 2, 2025 na kuongozwa na Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daudi Masasi kando ya Mkutano Mkuu wa wadau hao kutoka barani Afrika, unaofanyika jijini Dar es Salaam
Katika mazungumzo hayo, pande zote zimebainisha changamoto za ufadhili zinazoathiri utekelezaji wa programu za AMR, zikiwemo maeneo ya utafiti, uchunguzi wa maabara, elimu kwa umma, usimamizi wa matumizi ya dawa pamoja na ufuatiliaji wa mwenendo wa maambukizi sugu.
Msasi amesisitiza kuwa mafanikio ya juhudi za kupambana na AMR yanategemea mfumo madhubuti wa rasilimali fedha utakaowezesha afua kutekelezwa kwa ufanisi na kwa wakati.







Hakuna maoni:
Chapisha Maoni