Breaking


Ijumaa, 3 Aprili 2026

KAMATI YA USALAMA MAHALI PA KAZI BANDARI YA DAR ES SALAAM YAZINDULIWA


Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed tarehe 2 Aprili 2025 amezindua Kamati yaUsalama na Afya mahali pa kazi (OSHA)kituo cha Bandari ya Dar es Salaam katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Zimamoto na Usalama.

Akizindua kamati hiyo Bw. Abed amesema ni Kamati muhimu kwa kuwa ndio jicho la kwanza la TPA na Menejimenti kwani itasimamia na kuweka uangalizi ili kuzuia vihatarishi vya ajali na majanga na kuimarisha usalama na afya katika shughuli za uendeshaji bandarini.

Amesema kuwa Bandari ya Dar es Salaam ni kinara katika kuhudumia kiwango kikubwa cha shehena, hivyo ni tegemeo kiuchumi ikiwa pia ni sehemu yenye vihatarishi vingi, hivyo usalama na afya katika bandari lazıma upewe kipaumbele.


Naye Meneja zimamoto na Usalama Bw. Mussa Biboze, amesema kuwa kamati hizo zimeundwa kwa kufuata matakwa ya Kanuni na Sheria ya Usalama na afya mahala pa kazi zinazoelekeza waajiri kuhakikisha mahala pa kazi panakuwa na kamati za OSHA ili kusimamia usalama na afya wanapokuwa kazini.

Pia alitumia fursa hiyo kuwasihi wajumbe wa Kamati hızo kufanya Kazi kwa bidii ikiwemo kusimamia sheria za usalama na afya Bandarini kwa kuwa uwepo wake katika sehemu za kazi utazuia athari za ajali, majanga na kuimarisha Usalama afya zao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa DOWUTA Bandari ya Dar es Salaam Bw. Mashaka Karume, amesisitiza uwajibikaji katika kutekeleza majukumu na kutenda kazi kiuhalisia ili kuleta matokeo chanya katika kupambana na majanga yanayoweza kuepukika na kuweka mkazo katika kutekeleza majukumu waliyoaminiwa kuyasimamia.

Hakuna maoni: