Breaking


Jumamosi, 5 Septemba 2026

CHAMA AFUNGUKA KUHUSU JINSI ALIVYOJIUNGA NA YANGA



Kiungo wa Simba SC, Clatous Chota Chama, amefunguka kuhusu namna alivyohamia Yanga SC, akieleza kuwa wakati wa kusaini mkataba huo alikuwa hajawa tayari kuichezea klabu hiyo.

Chama amesema picha zilizotumika wakati wa kutambulishwa kwake Yanga zilipigwa hotelini wakati akisaini mkataba. Kwa mujibu wa maelezo yake, wakati huo alimweleza Rais wa Yanga kuwa hakuwa tayari kuichezea klabu hiyo na alikuwa tayari kurejesha kila kitu alichokuwa amepokea ili aendelee kubaki Simba.

“Niliwambia sipo tayari kucheza Yanga na nipo tayari kuwarudisha kila kitu chao ili nibaki Simba, lakini Rais wa Yanga alikataa,” Chama ameeleza.

Amesema mazungumzo hayo yalikuwa na mvutano mkubwa, huku akieleza kuwa Rais huyo alimweleza kwamba mashabiki na watu wengi walikuwa tayari wanamsubiri ndani ya Yanga. Hatimaye, Chama alisema aliamua kuheshimu mkataba aliokuwa ameusaini na kuendelea na safari yake ndani ya klabu hiyo.

Kauli hiyo imeongeza mjadala kuhusu kipindi cha Chama alipokuwa Yanga kabla ya kurejea Simba, huku mchezaji huyo akiendelea kueleza uzoefu wake kuhusu moja ya uhamisho uliokuwa ukifuatiliwa kwa karibu na mashabiki wa soka nchini.


Hakuna maoni: