Breaking


Alhamisi, 3 Septemba 2026

NDEJEMBI ATAKA BEI YA SARUJI ISHUKE HARAKA

Makamu wa Rais,  Deogratius Ndejembi, ameitaka Wizara ya Viwanda na Biashara kukaa na wazalishaji wa saruji kuweka mipango kuhakikisha saruji inapatikana kwa wingi na inashuka bei na kurejea ilivyokuwa.

Makamu wa Rais Ndejembi ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam baada ya kutoa tuzo kwa wazalishaji bora viwandani katika tuzo ya Rais ya Kwa Mzalishaji Bora Viwandani (PMAYA), inayosimamiwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).

Amesema hivi sasa watanzania wanalazimika kununua saruji kwa gharama kubwa kutokana na viongozi kushindwa kuratibu vyema uzalishaji wa bidhaa hiyo viwandani.

“Haya yanasababisha uhaba wa saruji na anayeumia hapa ni mtanzania wa kawaida na serikali hii ya awamu ya sita ya daktari Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake anataka kuona mtanzania anapata mfuko wa saruji kwa gharama nafuu,” alisema na kuongeza

“Sasa nakuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara namwona hapa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kanei pamoja mmalize hili suala ili mtanzania apate saruji bei iliyokuwepo,” alisema.

Aidha, alisema mchango wa sekta ya uzalishaji katika pato la taifa  mwaka 2025 ulifikia asilimia 5.9  na kwamba inakadiriwa kuwa asilimia 12 ya ajira rasmi na bidhaa zilizokuwa zinauzwa nje zilikuwa za viwandani.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), Leodegar Tenga, alisema 

PMAYA inalenga kutambua, kuthamini na kuenzi mchango wa sekta ya viwanda katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Hakuna maoni: